Ujumbe toka DRC wafurahishwa, utendaji kazi wa Bandari

Ujumbe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ulifanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam mapema wiki iliyopita na kelezea kuridhishwa kwake na uendeshaji wa shughuli katika bandari hiyo. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, mkuu wa ujumbe huo, Gavana wa jimbo la Katanga nchini DRC, Jean Claude Kazembe Musonda alisema walifurahi kuwa baadhi ya changamoto zilizokuwa zinaikabili bandari katika kipindi cha miaka ya nyuma yametatuliwa katika miezi ya karibuni. “Tuna furaha kuona baadhi ya changamoto zilizokuwa tunazilalamikia zimetatuliwa na mizigo yetu inapewa kipaumbele katika bandari. Tunataka kuona mahusiano yetu ya kiuchumi yanakuzwa na kuboreshwa kwa maendeleo ya watu wetu,” alisema.

Mr Masundo Aliongeza kuwa asilimia 50 ya biashara za DRC hupitia bandari ya Dar es Salaam na kwamba wanapanga kuendelea kutumia bandari hiyo kutokana na usalama wake, ufanisi wake na ukaribu uliopo kati ya Tanzania na DRC. Mr Musonda alisema kuwa kuna mipango inaendelea ya kujenga madaraja ambayo yataimarisha mahusiano ya kiuchumi kati ya nchi tatu za Tanzania, DRC na Zambia.

“Katika ziara yetu Tanzania tulikutana na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof Makame Mbarawa, kujadili ujenzi wa daraja utakaogharimu dola za Kimarekani milioni 85. Daraja hilo litasaidia kuongeza ushirikiano wa kibishara kati ya Tanzania, DRC na Zambia ,” alisema.

Alitoa wito kwa nchi nyingine jirani kuendelea kutumia bandari ya Dar es Salaam kwasababu changamoto nyingi zimetatuliwa.

No Comments

Post a Comment