TATOA yawasilisha matatizo yake kwa Waziri Mkuu

Mwenyekiti wa TATOA Bi. Angelina Ngalula wiki iliyopita alihuduria mkutano uliomkutanisha Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa na wadau mbalimbali wa sekta binafsi nchini. Maswala mbalimbali yanayoihusu TATOA yaliwasilishwa na kujadiliwa katika mkutano huo. Maswala hayo ni yale yanayogusa uendeshaji wa kila siku wa biashara za wanachama wetu hasahasa zile zinazosababisha matatizo katika biashara zetu.
Akiongea katika mkutano huo, Bi. Ngalula aligusia swala la malipo ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT) katika   huduma ya usafirishaji wa mizigo iendayo nje ya nchi, swala ambalo lina athiri gharama za utoaji wa huduma kwa wasafirishaji wa Tanzania. Pia katika mkutano huo, matatizo yanayokabili Himaya ya Umoja wa Forodha (Single Customs Territory) hasahasa ile na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yalijadiliwa. Maswala ya  ucheleweshwaji wa mizigo mipakani, ufinyu wa maeneo ya kuegesha malori karibu na bandari na katika miji mbalimbali malori yanapopita yakiwa yanasafirisha mizigo pia yaliwasilishwa na kujadiliwa katika mkutano huo. Pia swala la wembamba wa barababara katika mipaka ya Tanzania lilijadiliwa. Barabara za mipakani zina wembamba wa kupitisha gari moja kila upande, jambo linalosababisha foleni ndefu ya malori.
Mheshimiwa Waziri Mkuu amewasilisha maswala yote yaliyojadiliwa katika kikao hicho kwa mawaziri wa wizara stahiki na akaahidi kuitisha mkutano mwingine hivi karibuni utakaohudhuriwa pia na mawaziri wa secta hizo zinazolalamikiwa watakaotoa majibu stahiki ya maswala yote yaliyowasilishwa.
Tutaendelea kuwataarifu wanachama wetu jinsi jambo hili litakavyokuwa linaendelea.

No Comments

Post a Comment