TATOA kuwasilisha mapendekezo ya marekebisho ya sheria mbovu za kodi

TATOA ikishirikiana na wadau wengine iko kwenye maongezi na kampuni ya ushauri ya kodi ya Price Waterhouse Coopers (PWC) kwaajili ya kutengeneza mapendekezo ya kuangaliwa upya kwa baadhi ya sheria za kodi zinazokuwa mzigo kwa uendeshaji wa sekta yetu ya usafirishaji hasahasa sheria zihusuzo kodi ya ongezeko la thamani. Mapendekezo hayo yanaandaliwa kwa kwa nia ya kuyawakilisha serikalini.
Kwa muda sasa kumekuwa na malalamiko juu ya sheria mbalimbali, hasahasa vifungu vidogo vya sheria zinazopingana na sheria mama katika utekelezaji. Mfano mmoja ni sheria mpya ya kodi la ongezeko la thamani (VAT) inayotaka kampuni za usafirishaji kulipa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye bidhaa zinazosafirishwa kwenda nje ya nchi pale kampuni iliyopewa kazi ya usafirishaji inapoipa kampuni nyingine kazi hiyo (subcontract). Sheria mama ya kodi la ongezeko la thamani inasema kwamba VAT inachajiwa kwenye bidhaa na huduma zinazotumika ndani ya nchi pekee. Bidhaa na huduma zinazotumika nje ya nchi hazilipiwi kodi ya ongezeko la thamani na hivyo kwenye mfano huu, malipo ya kodi la ongezeko la thamani  yanaenda kinyume na sheria mama ya kodi.
Wanachama mtahabarishwa maendeleo ya mchakato huu.

No Comments

Post a Comment