Taarifa kwa wanachama ya mchango wa secta ya elimu na afya

Katika hotuba yake aliyoitoa alipokuwa anazungumza na wazee wa Dar es Salaam tarehe 13 mwezi wa pili 2016, Raisi Dr John Pombe Magufuli aliahidi kutoa sehemu ya mshahara wake kuchangia huduma ya elimu bure katika mkoa wa Dar es Salaam; ambao umeshuhudia wimbi kubwa la wanafunzi wakijiandikisha katika mashule. Hili limetokana na uamuzi wa serikali ya awamu ya tano kufanya elimu ya msingi kuwa bure. Wimbi hili la wanafunzi wapya limesababisha tatizo la ufinyu wa madarasa, madawati na hata vitabu vya kufundishia mashuleni.

Ili kuungaa mkono jitihada za mheshimiwa Rais Dr John Pombe Magufuli, TATOA inapenda kuwaomba wanachama wetu wote kuunga mkono hatua hiyo ya mheshimiwa Rais kwa kuchangia kwa hiari mfuko ulioanzishwa na chama kwa madhumuni hayo. Michango itakayokusanywa itatumika kuunga mkono jitihada za serikali kwa kununua vifaa vya muhimu kwenye elimu kama vile madawati, vitabu na pia itatumika kusaidia ujenzi wa madarasa kwa kununulia vifaa vya ujenzi. Pia chama kitaunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha sekta ya afya nchini kwa kuchangia vitanda vya hospitali, magodoro na vifaa vingine vya muhimu kwenye utoaji wa huduma za afya. Kampuni zote zitakazochangia mfuko huu watatambuliwa rasmi na majina yao kukabidhiwa serikali kama ishara ya kuthamini michango yao. Pia kampuni hizo zitakaribishwa kwenye shughuli ya makabidhiano na serikali kama watapenda kushiriki. Vyeti vya shukrani vitatolewa.

Michango yote iwasilishwe kwa njia zifuatazo:
  1. Moja kwa moja kwenye ofisi zetu Pugu Road ambapo risiti itatolewa.
  2. Kwa kutuma kwenda M-Pesa (0754411148)/ Tigopesa (0713411148)
  3. Kwa kuweka kwenye akaunti yetu katika benki ya Stanbic; nambari ya akaunti 0140005088001 lenye jina la TATOA.
Tunawashukuru.

No Comments

Post a Comment