Mrejesho kuhusu swala la C28

Tarehe 23/1/2017 bodi a TATOA ilikaa kwenye kikao cha ndani kuzungumzia swala la tozo ya C28 ambayo TATOA imekuwa ikitaka zishuswe tangia zitangazwe kuongezwa kutoka Tsh 20,000 mpaka $200 USD. Bodi, ikizingatia kwamba mwisho wa mwezi wa kwanza ulikuwa umekaribia na hivyo mwisho wa nyongeza ya muda iliyotolewa na serikali kuendelea kutumia leseni ya mwaka jana ya C28, ikaona vyema kutoa msimamo wake wa jambo hili.

Bodi ya TATOA inaendelea na jitihada zake kuzunza na serikali ili au kupunguza kiwango cha tozo za malipo ya leseni ya C28 au kuondoa malipo wakati wa kutengeneza upya (renew) leseni ya C28 zaidi ya mara moja kwa mwaka au kufanya kama nchi nyingine za Afrika Mashariki zilivyofanya kwa kuondoa moja kati ya malipo ya C28 au malipo ya vingamuzi vya magari. Hata hivyo, kutokana na maongezi na serikali kutokutoa mwafaka kabla ya January 31, TATOA inawashauri wanachama wake kulipia leseni ya C28 kwa baadhi ya magari yao ili waweze kuendelea kufanya kazi wakati bodi ikiendelea na mazungumzo na serikali ili kupata suluhisho la kudumu.

Ni imani ya TATOA kwamba serikali itasikia kilio chetu na dhamira yetu ya kujenga nchi kwa pamoja. Tutaendelea kuwajulisha wanachama wetu kadri mazumzo yatakavyokua yanaendelea.

No Comments

Post a Comment