Kituo cha pamoja cha forodha Tanzania – Zambia chazinduliwa

Kituo cha pamoja cha forodha cha mpaka ulioanzishwa kati ya Tanzania na Zambia na kuanza operesheni tokea Februari 1 2017 katika mpaka wa Tunduma-Nakonde utapunguza na kukuza biashara kati ya nchi hizo mbili, viongozi waandamizi wa nchi hizo mbili wameeleza. Nchi hizo mbili tayari zimeshasaini makubaliano ya namna umoja huo wa forodha tavyofanya kazi.

Uamuzi wa kuanzisha umoja huo wa forodha ulikuja kama sehemu ya utekelezaji wa agizo iliyotolewa na marais wa nchi hizo mbili, John Magufuli na Edgar Lungu. Viongozi hao wawili walitoa amri jijini Dar es Salaam wakati Rais wa Zambia Lungu alitembelea Tanzania mwezi uliopita. Sherehe ya kutia saini makubaliano hayo ulifanyika katika mji wa Vwawa uliopo kilomita chache kutoka mpaka wa Tunduma-Nakonde, ambapo Tanzania iliwakilishwa na Amina Khamis Shaaban, Naibu Waziri wa Fedha na Mipangoi na Adolf Mkenda, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji. Zambia iliwakilishwa na Kayula Siame, katibu mkuu wa wizara ya Biashara, na Viwanda.

Mh Amina Shaaban alisema kuwa umoja huo wa forodha utarahisisha ufanyaji biashara kati ya nchi hizo mbili. Alieleza kwamba umoja huo wa forodha umeanzishwa ili kupunguza gharama za usafirishaji kati ya nchi hizo mbili kwa kuunganisha shughuli za mipaka ya nchi hizo mbili kufanyika sehemu moja.

Aliendelea kuelezea kwamba utaratibu juo mpya utaleta unafuu kwa wafanyabiashara kwa mzigo kukaguliwa mara moja tu badala ya utaratibu wa zamamni ambao mzigo ulikuwa unakaguliwa mara mbili. “Hii itawezesha pia kuongeza makusanyo ya mapato,” alisema Naibu Waziri na kuongeza: “Kituo hicho pia kitashughulikia changamoto zote ambazo zimekuwa zikikwamisha bisahra kati ya nchi hizi mbili. Itahamasisha wafanyabiashara wa nchi hizi mbili kufanya biashara pamoja. ”

Mh Amina pia alielezea matarajio ya serikali kwamba kituo hicho pia kitasaidia kupungua kwa magendo ya bidhaa katika mpaka wa Tanzania na Zambia. “Kituo hiki kitaleta pamoja taasisi za nchi hizi mbili kufanya kazi kama timu moja, kitu kitakachowasaida kubadilishana uzoefu utakaosaidia kuboresha shughuli zao za siku hadi siku,” alisema.

Naye Bwana Mkendaalieleza kuwa uboreshwaji wa huduma katika mpaka utaongeza biashara ya usafirishaji wa mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam kwenda Zambia na nchi nyingine jirani. Charles Kichere, Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), alisema kituo kitakuwa na vifaa vya kisasa vya mawasiliano ya habari na teknolojia (ICT).

Kwa upande wake, mwakilishi wa Zambia alisema kuwa wananchi wa nchi hizo mbili wanatakiwa kuchangamkia fursa itokanayo na kituo hicho kuongeza ufanyaji biashara kati ya nchi hizo mbili. Kituo hich cha umoja wa forodha ni cha tano kuanzishwa baada ya zile zilizopo kati ya mpaka wa Tanzania na nchi jirani za Kenya, Uganda, Rwanda, na Burundi.

No Comments

Post a Comment